MOTIVATION CORNER
Madam Violet Konyani
FOUNDER WOMEN POWER FOR DEVELOPMENT ORGANIZATION
HESHIMU NDOTO YAKO, ITUNZE IKUE.
Kila mtu Mungu amempa upekee wake, maono yake na ndoto yake. Yaani mimi siweze kulala nikaoteshwa maono ya @Da Aiyana au maono ya @Christina Bianchi, kila mtu Mungu anampa kuota kulingana na kile ambacho Mungu anakihitaji kutoka kwake. Ninachokiamini mimi ni kwamba kila mtu anapambana kweli ili aweze kutembea kwenye njia yake. Kama kuna mtu amesimama anasubiri muujiza bila kujitafuta ni lazima kutakuwa kuna shida mahali. Mungu akufungue macho uone vyema kama siyo uone sawasawa.
Na wale ambao tayari tunaziishi tujifunze kwamba zipo nyakati tutapita tena nyingine ni za maumivu makali sana lakini lazima tufike. Ndugu yangu mmoja huwa anasema mapito hayo badala yakulize, yakusanye yawe nguvu ya kukuongezea bidii.
📌Ndoto hupitia wakati wa ukimya.
Huu ni wakati ambao nguvu zako zitakuwa hazilingani na matokeo unayoyapata. Wakati huu hutokea kwa sababu ni wakati wa mbegu kukusanya nguvu ya kuchipua. Ni kama vile wale wafanya mazoezi jamani huwezi kupungua siku moja kila siku unavyoongeza jitihada ndivyo ambavyo unazidi kukua. Au wewe ni mkulima mbegu ikiwa haijaota haimaanishi imekufa unatakiwa kuendelea kuitunza hata kama hakuna unachokiona kwa juu. Sasa wapendwa, hapa huwa hatuachi eti kwa sababu huoni kitu, huu ni wakati tu, unachotakiwa kufanya ni kuendelea mbele bila kuchoka. Ukiwa mtu wa kuchoka kwenye hii hatua ya kwanza tu nguvu zikiisha maana yake safari yako imeishia hapa, kitu ambacho hakikuwa nia wala matamanio yako.
📌Ndoto hupitia wakati ambao kila mtu hakuamini.
Kuna wakati kila mtu anakuwa na mashaka na unachokifanya. Japokuwa wewe mwenyewe unaona unachokifanya kwa sababu wewe ndiye mwenye matamanio na ndiye unaijua safari yako na una uhakika huko mbele yapo mazuri zaidi. Utashangaa kila anayekuzunguka hakuamini. Kila mtu anasema lake. Kila mtu anashauri lake. Lakini wewe kila ukichekecha akili yako unabaki kuwashangaa kwani hawa ni vipofu au?
Nasema hivi ndoto yako ikifika mahali kila mtu hakuelewi ndio wakati sahihi wa kufanya zaidi ili uendelee kumshangaza mwovu shetani. Mi sijui wewe unafanya nini ila ndio nakupa hizo hatua. Pima kwako ina apply vipi, songesha gurudumu lako kazi iendelee.
📌Ndoto huwa inapitia wakati wa kuchoka. Kuna wakati unafika nguvu ambazo ulikuwa nazo za kupambania ndoto yako hautakuwa nazo tena, itakuwa kama vile umepoteza hamasa ya kupambana. Yani kuna ule wakati unafika unasema natamani kama liwalo na liwe tu nimechoka. Unatamani kuanza kitu kingine, tena kinakujia kila saa.
🔖Ndugu yangu hatufanikiwi kwa sababu hatuna nguvu za kufanya. Tunafanikiwa kwa kujilazimisha kuendelea kufanya.
Muendelezo ndio njia pekee ya mafanikio.
Unaweza ukawa kwenye maumivu lakini kila ukipiga jicho mbele unasema lakini naiona kesho njema sana lakini mbona nguvu sina? Shetani amekaa pembeni anasema mbona huyu anachelewa kuacha. Hakikisha unasimamia jambo lako unaloliamini mpaka linafanikiwa. Wewe ndio uliyeanza na ulijua kwanini umeanza. Kupita pagumu ndio kujua kwenyewe na kujifunza zaidi. Leo ukitembea peku ukakanyaga msumari utakumbuka umuhimu wa kuvaa viatu. Nikutie moyo ndugu yangu, mimi sijui wewe uko wakati gani pambania chako bila kuchoka wala kukata tamaa. Mungu hajakupa karama yako kwa bahati mbaya. Amekutuma ufanye kazi. Ukirudi kwake ukampe majibu yake.
Najua upo wakati tunapita kwenye magumu sana sana tu. Huo ugumu ndio ukuaji wenyewe.
📍Hatuwezi kuvuka kwenye changamoto kama hatujakubali kuwa zipo, akili yako lazima ikubali kuwa hiki ninachokifanya changamoto nitakutana nazo tu zisiwe kiwazo cha safari yangu.
📍Ukiona changamoto zimezidi usiwakimbie watu tafuta msaada uinuliwe, kumbuka unachokifanya chochote wapo watu wanakifanya, pia omba ushauri kwao ili uendelee mbele. Watu wazuri wapo na wako tayari kukusaidia usiue kitu kabla hujakipambania. Kuna wakati tunaweza kabisa kuwa na vitu vizuri lakini haviendi labda hatukuanza kwa wakati sahihi au hatukushirikisha watu sahihi. Lakini ni muhimu sana kuusikiliza moyo wako kila wakati, ukiwa na moto wa presha nyingi za watu huko nje unaweza jikuta umeshindwa kufanya kila kitu.
📍Hakikisha unaheshimu ndoto yako, unaitunza na inakua usikubali kufia njiani.
Tengeneza misingi imara uweze kujiimaarisha zaidi. Tengeneza misuli ya ukomavu kutetea kilicho ndani yako. Hicho kiko ndani, ndio maana watu wa nje ni ngumu sana kukiona. Kulinda misingi ya mafanikio yetu wapendwa wangu ni muhimu mno. Changamoto yetu wengi ni kutaka mafanikio bila kuwa na misingi imara na matokeo yake tunapanda kwa muda mfupi tunatakata tamaa tunapoteza kila kitu. Kuna wakati bora uchukue muda mrefu kujenga misuli yako iwe imara kulingana na kazi yako kuliko kufanya kwa papara dunia ijue kumbe unajimaliza mwenyewe. Wazungu wanasema “your public value is the product of your private investment.” Kabla hujataka kuwa bora kuliko kila mtu nje, jitahidi kuwa bora kuliko kila mtu wakati hakuna anayekuona. Kufeli kupo lakini kufeli sio sababu ya kukufanya usiendelee. Mtu anaweza badilisha muelekeo na akatengeneza safari nzuri sana akiamua.
Yapo mambo mengi yanaweza kutokea njiani na yakasababisha safari yako kuwa ngumu sana, badala ya kukaa pembeni na kuanza kulalamika jiulize ni kitu gani kingine naweza kufanya? Then fanya. Usikubali kuwa mtu wa kukaa kaa tu kisa ulifeli. Hapana kila siku akili yako iwe sharp kuhakikisha unaendelea mbele.
📍Huwezi kukuza ndoto yako ukiwa umekumbatia kila aina ya vitu, vingine ni vizito vitakuangusha. Kubali mengine yapotee wewe ukue. Hata kama ni watu sawa tu. Lazima tujue kila mtu akija kwenye maisha ana sababu. Kuna atakayekuja kukaa. Kuna atakayepita.
Kuna atakayekuja kuongeza thamani halafu akaenda zake. Kuna wengine inabidi waondoke ili uanze kujitambua. Njia ya kuiishi ndoto ina mengi sana. Kelele zote hizi ni kutaka wewe usikate tamaa kwenye hatua yoyote ambayo upo sasa. Hata watu watakao kukataa, jua ipo faida kwenye kukataliwa pia. Na mara nyingi watu wetu wa karibu ndio wepesi kutukatisha tamaa kwa sababu wanatujua, wanajua madhaifu yetu. Usikubali, funga dirisha lako mtafaana mbele huko.