MOTIVATION CORNER
By Mariam Kisimbe
Advocate/Conflict Resolution Consultant
HEKIMA YA MAPOKEO
Kwa kawaida neno mapokeo tumekuwa tukilisikia kutokea nyumba za ibada na hasa kanisani. Lakini kupokea kwenye jamii yetu ni neno ambalo limekuwa likitumika (kitenzi) kumaanisha kufanya jambo fulani ambalo limekuwa likifanyika huko nyuma na wakubwa au watangulizi hivyo limepokelewa kama lilivyo na linafanyika kama lilivyo bila kubadilisha wala kupunguza.
Maana nyingine ya mapokeo na hasa ambayo tutaimaanisha hapa ni kupokea ambako kunahusisha kulikaribisha jambo au kitu na ukalipatia umuhimu wake unaostahili. Kupokea kwa maana ya kulikaribisha au kulikubali jambo fulani ndio mzizi wa somo letu la leo. Kupokea kwa maana ya somo hili ni kusikia, kusikiliza na kupitisha kwamba sasa hiki nilichoambiwa ni changu mimi au la!
📌Kwa nini somo hili?
Tupo kwenye wakati ambao tunapokea taarifa nyingi sana kwa uharaka na kwa namna ambayo haina mpangilio maalumu. Tupo kwenye wakati ambao mtoa taarifa au kitu fulani hajali wala hana haja ya kujiuliza ninayemwambia yupo kwenye hali gani au atapokea vipi hizi taarifa?
Zamani kidogo hivi mpaka miaka ya 90 mwanzoni ilikuwa ikitokea msiba anatumwa mtu aende mahali fulani kutoa taarifa na hakuwa anatumwa mtu tu bali yule mwenye uwezo wa kutulia na anayeweza kutoa taarifa kwa usahihi bila kuleta taharuki. Na haikuwa kirahisi hivyo, wakubwa walifikia hatua kwamba anachaguliwa mtu wa kumtuma kulingana na ukubwa wa msiba. Kama kafariki ghafla mtu mzima ambaye kwenye jamii anahitajika sana na ni mhimili wa walio wengi anatafutwa mtu mzima mwenye akili timamu ndio akatoe. Ikibidi watu wanaitwa bila kutoa taarifa ya msiba mpaka wakutane ndo wajue nini ni nini.
Kwa upande mwingine, Mnafikiri zamani hapakuwa na watu wanatoka kwenye ndoa zao? Kwani hawakuwa wanafumaniwa na kufumaniana? Lakini taarifa inavyotoka ni kwa staha sana kiasi kwamba inaweza kulinda hadhi sio tu ya wahusika bali wale wanaopokea walikuwa wanalindwa pia.
Kila mmoja anatakiwa kuwa daktari wa nafsi, roho na mwili wake. Lakini muhimu kwa leo tunakazania udaktari wa NAFSI yako. Maana nafsi ndio inayopokea hisia na inapokea taarifa nyingi sana. Wapendwa wangu sisi ni binadamu…Binadamu yeyote ni mbinafsi na angependa kujiridhisha mwenyewe kwanza. Kila kitu kizuri binadamu atataka kiwe chake kwanza kabla hakijaenda kwa wengine. Binadamu ni mbinafsi sana na ni asili hivyo hawezi kukuchujia wewe taarifa hata moja. Yeye atafanya kwa nafasi yake anavyoona ni sawa wewe unayepokea jiandae kumeza au kuitema.
Kuna mwalimu mmoja alimpigia simu mzazi akimpatia taarifa ya wito wa haraka shule, akamwambia “Hello! Wewe ni Mama fulani? Jumatatu asubuhi njoo shuleni mwanao ni shoga!” Mzazi akauliza “ee mwanangu shoga?” Mwalimu akajibu “ndio anafanya mapenzi na wanafunzi na amewaharibu watoto wa watu wengi.”
Sijui mnaiona hii taarifa??!!
Mtoto ambaye ni mpole na mzazi wake hajawahi kumtilia hata shaka achilia kwenye hayo mambo, pia sio kijana wa mambo mengi.., taarifa zikaja mbili kwa wakati mmoja ‎1. Ni shoga 2. Anaharibu watoto wa watu. Mama wa watu akaanza kutetemeka anatamani aende shule muda huohuo! Hata amuulize huyo mwalimu wa nidhamu ni nini kinaendelea, mwalimu hapokei tena simu.
Lakini si kulikuwa na namna nyingine ya kumuita? Ilikuwa na umhimu upi wa kuyasema yote hayo?? Na ujue ilikua ni Ijumaa asubuhi, mtoto sio wa kulala bweni anarudi nyumbani. Mama anajiuliza aongee naye? Lakini hana taarifa kamili.
Je akiongea naye nusu nusu mtoto atajisikiaje?
Wapendwa, hizi hali haziepukiki!! Kifanyike nini kwenye ulimwengu huu ambao mtu anaweza kukuambia chochote? Mtu hajui umekula mara ya mwisho lini anakutana na wewe pap, anakwambia punguza tumbo Mariam au umenenepa sana siku hizi. Au mbona umepungua sana yaani umepauka kuna usalama huko? Mtu hamjawahi kukutana miaka na miaka tangu utoto wenu leo mnakutana anakuuliza watoto hawajambo?
Pengine unahangaika kwa waganga na waganguzi kutafuta watoto. Ndio kwanza talaka imetolewa majuzi unatafuta kupona mtu anakuuliza “Mr. hajambo? Ndoa imekupenda.”
Kwanza kabisa kama binadamu jiandae tu, mtu anaweza kukuambia chochote kwa namna yoyote. Utulivu ni nguzo muhimu sana. Kuna mtu aliwahi kusema ukiwa mtulivu unaweza kulala na maiti hata siku 3 na maisha yakaendelea.
Utulivu una ngazi tatu:
1. Kusikiliza
2. Kutafakari
3. Kupokea
Tunaona kupokea ni hatua au ngazi ya 3 na ya mwisho. Ukiiweka mbele utaumia.
Sasa kuelewa hapa turudi kwenye mapokeo ya kanisani wale wa Roma na Lutherani mnafahamu. Na ndio maana kwa kizungu kupokea wanaita CONFIRMATION. Si ndivyo keki za watoto siku ya kupokea zinavyoandikwa? Hakuna anayepokea bila kuthibitishwa kwamba anapokea anachokifahamu. Lazima usomeshwe kwanza, Uelewe unachoenda kupokea, kisha upokee. Maana yake ni nini? Hata taarifa ya msiba ikija sio lazima uibebe kwa namna ile tunabebaga.
Dawa yake hii hapa;
1.Sikiliza tena kwa makini sana…, kama taarifa ni nusu hata jirani yako hatakiwi kusikia.
2.Tafakari kwa kina kwa nini taarifa ije kwako? Wajibu wako nini kwenye hiyo taarifa na utatimizaje huo wajibu kama upo?
3.Kisha pokea kwa ajili ya utekelezaji. Sio kila taarifa unatakiwa kuifanyia utekelezaji. Lakini ukipokea kabla hujatafakari lazima utajikuta unaifanyia utekelezaji ambapo lazima uchemshe tu.
Lazima ufahamu mtoa taarifa ana kusudi gani na wewe kwanza.
Tunaumizwa sana na vitu ambavyo hatukuchagua viwe hivyo au hatuna mamlaka ya kuchagua. Ni kosa kubwa sana. Wewe ambacho kinatakiwa kukuumiza na ukakipokea kwa namna hiyo ni kile ambacho umechagua na una mamlaka nacho au ulikuwa na mamlaka ya kufanya tofauti na vile.
*Chagua aina ya changamoto zako*
Tumepewa mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka. Sio lazima kila kitu kiwe sehemu ya maisha yako. Habari ya msichana wako wa kazi kutembea na mumeo sio changamoto yako. Kwa sababu msichana wa kazi unamlipa wewe na vigezo vya kuwepo kazini vinajulikana sioni kama kuna mjadala pale ambapo mtu kavunja masharti ya mkataba. Una sababu ya kumsimulia aliyekuletea? Aliyezaa nje swali sio kwa nini umezaa nje maana mtoto alishazaliwa, bali ni kutafuta akili ya kuweka mipaka huyo aliyezaliwa hasiharibu usitawi wa walioko ndani.
Nimeenda milembe juzi kati tunaambiwa vichaa wengi wa kike hivi karibuni ni sababu ya ndoa na mahusiano. Nikajiuliza sana sana.
Na ndio maana unaweza kuja kwangu na jambo lako zito nikakupa jibu moja tu, “Hii changamoto sio yako unalazimisha tu ije kwako.” Usipambane kubeba stress za wenzako. Chambua kwamba hii ni yangu au ya wengine? Ukijua sio sehemu ya changamoto yako shika jembe ukalime.
Badilisha mtazamo wako. Badala ya kukaa kwenye kupambania ulichosikia au kupewa taarifa zingatia kile unachoweza kudhibiti kwa sasa. Kimeondoka nini na kimebaki nini? Jiulize hilo swali wakati wa kutafakari. Hakuna kisichowezekana chini ya jua. Na hakuna changamoto ambayo haina utatuzi. Wakati unajimaliza kumbuka hiyo hali haiwezi kudumu maisha yako yote. Sema sasa utabaki nayo mpaka lini ni maamuzi yako tu. Unaweza kukubali mtu achukue vyote leo tena haraka haraka ili upate muda wa kutafuta vingine. Unaweza ukakubali kuwaondoa uliowapenda na kuwaamini haraka haraka kwenye maisha yako ili waje ambao wanakupenda pia haraka haraka. Unakubali kusamehe haraka sio kwamba ni ujinga au upumbavu bali unataka nafasi ya kufanya mambo mengine kwa haraka haraka na hauna nafasi ya kubeba sana.
Sisi waislam mtu akifariki ni sharti asikae sana. Yaani kama inawezekana afe na kuzikwa palepale. Sio tu kwa ajili ya aliyefariki bali kuwapa nafasi hata wale ambao wanaomboleza. Sio watu siku 5 hawajazika wanasubiri kaka wa Marekani afike. Waliopo eneo la tukio wanalia mpaka wanatundikiwa drip maana wanaona mwili wa mpendwa wao hapo.
Unakubali kuachilia sio sababu ni rahisi au hujaumia, bali unajifanyia usafi wa mahali pa kukaa baraka. Nafsi ikikaa na migogoro hakuna kinaweza kueleweka maana hata mbili utaiona ni nane.
Mwisho, jikumbushe kuwa hali nyingi ni za muda na kwamba uwezekano wa kuzishinda unao wewe. Jaribu kuiona kwa mtazamo mpana. Jamani mbinu hizi zinaweza kusaidia katika kusitawisha utulivu, lakini zinaweza kuchukua muda sababu kuna kitu kinaitwa mazoea. Usisahau pia nafasi ya Mungu katika haya yote. Lakini lazima tuweke mizizi ambayo itasaidia kuleta mabadiliko chanya kwenye kila tunachofanya. La sivyo kazi tutafanya lakini tutakosa matokeo ambayo tulitarajia.
Nawakumbusha kwamba kupokea kwa maana ya somo hili ni kusikia kusikiliza na kupitisha kwamba sasa hiki nilichoambiwa ni changu mimi.